Judegment Day At The High Court London

Judegment Day At The High Court London
Mengi v Hermitage: Libel Claim Successfully Defended

Tuesday, 23 August 2011

Kisa cha shamba la Silverdale: Je Tanzania inatisha wawekezaji?

 

http://www.corruptiontracker.or.tz/dev/index.php?option=com_content&view=article&id=178%3Asiverdale-farm-case-is-tanzania-scaring-investors&catid=18%3Acurrent-issues-&Itemid=51&lang=br

“Hupaswi kukubali kuwa rushwa ipo na badala ya kupambana nayo ukafanya kinyume chake kwa kuikubali. Unapaswa kupambana na rushwa kwa nguvu zako zote kwa kuhakikisha unaandaa mipango ya kuitokomeza.

Inapaswa kukumbuka kuwa kiini cha sera yoyote ya misaada au mambo ya nje ni kutuzuia kuwa mashabiki wa vitu ambavyo vinaweza kutokomeza taifa letu, ukumbatiaji wa rushwa ukiwa ni moja ya vitu hivyo,” hayo yalisemwa na Mstahiki Jay wa Ewelme, mwenyekiti wa Kamati ilivyochaguliwa katika kusimamia masuala ya kiuchumi Julai 5, 2011.

Mnamo Julai 19, 2011, Kamati ya Maendeleo ya Kimataifa ilipoendesha kikao cha wazi cha ushahidi ambapo maafisa toka Idara ya kimataifa ya maendeleo (DfID), BAE Systems na Kitengo cha kushughulika na uhalifu mkubwa “Serious Fraud Office (SFO)” ilitoa ushahidi wa matamshi juu ya hatma ya paundi milioni 29.5 za Uingereza ambazo BAE Systems imekubali kulipa kwa maslahi ya watu wa Tanzania katika kufidia ongezeko la gharama katika uuzwaji wa rada.

Msukumo unashinikizwa kwa serikali ya Uingereza kurejesha fedha hizo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania (zikiangaliwa na DfID) na si katika mashirika yasiyo ya kiserikali.

Fedha za BAE zisipelekwe moja kwa moja katika serikali ya Tanzania. Nina endelea kujenga hoja, baadhi ya fedha za DfID zinatumika vibaya Tanzania, idara hiyo inaweza isimudu kuzisimamia na kuripoti fedha ambazo zitaletwa toka BAE. “DfID inaweka fedha nyingi (na imani) katika programu ya Msaada wa Pamoja wa Bajeti “General Budget Support”. Katika hali ya bajeti kuwa yenye uhanga wa kuliwa na kupotea, kwa mantiki hiyo fedha za DFID zinapotea” (1)

Rushwa ni ugonjwa sugu Tanzania. Profesa Robert Picciotto wa chuo cha Kings London hivi karibuni alitaja katika kamati ya Uchumi ya mabwanyenye, bunge la Uingereza (House of Lords Economic Affairs committee) kwamba “……kujenga uwezo wa Taifa imedhihirika kuwa ni muhimu, hasa kujenga taasisi za masoko, utawala wa kisheria na ulinzi wa haki za mali ambapo sekta binafsi inategemea”.

Licha ya misaada lukuki kwa Tanzania, uzoefu wetu unaaminisha kuwa serikali ya Tanzania katika kujidhatiti na kuenenda kwa mujibu wa utawala wa kisheria hususan katika masuala ya ardhi na haki ya mali.

Kilichotutokea kwetu nchini Tanzania kilikuwa cha kinyama na kiliwezeshwa, kwa namna fulani na serikali.

Utawala wa kisheria Tanzania ulishindwa wazi kutusaidia. Kesi yetu na nyingine zinaonyesha kiini cha tatizo katika fursa ya kupata haki na kulindwa kwa haki za kibinadamu nchini Tanzania.

Muono huu unaungwa mkono na ripoti ya haki za kibinadamu ya mwaka 2009 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu.

Mnamo mwaka 2009, shirika la Transparency International (Utafiti wa hali ya Rushwa Afrika Mashariki) ilizitaja Mahakama Tanzania kushika nafasi ya nne katika taasisi vinara kwa rushwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, na ripoti ya mwaka 2010 ya Idara ya Marekani inayohusika na Haki za Kibinadamu ilitangaza mahakama nchini Tanzania kutawaliwa na “rushwa na kukosa ufanisi”.

Ripoti ya mwaka 2009 ya Freedom House juu ya Tanzania iligundua katika kesi ambazo zilihusisha hukumu ya mali binafsi (kama ilivyokuwa kwa kesi ya shamba la Silverdale) mahakama isingekuwa ya kutegemewa kusimamia katika sheria na haki na hapo ndipo maslahi ya wenye uwezo wa kifedha na nguvu za kisiasa inashika hatamu.

Kuna tafiti nyingi toka katika taasisi za kitaaluma zenye kuheshimika katika eneo ya hali ya rushwa nchini Tanzania, zikiwemo zile zinazochapwa na shirika la DfID chini ya programu ya Afrika, Nguvu na Siasa na hususan tafiti iliyofanywa na Brian Cooksey na kuitwa; Mali za umma, pango na biashara nchini Tanzania (Public goods, rents and business in Tanzania).

Kituo cha taarifa za kupambana na rushwa cha U4 Anti-corruption inamtaja Mkaguzi Mkuu wa Tanzania akisema, si chini ya asilimia 20 ya matumizi ya serikali yanapotea katika rushwa nchini Taznania, na inajidhihirisha wazi wazi rushwa inazidi kuwa katika hali mbaya kuliko kuwa katika hali nzuri.

Tanzania imeshuka kwa nafasi 23 katika tafiti juu ya mtazamo katika rushwa iliyotolewa na shirika la Transparency International katika miaka minne iliyopita (ilikuwa nafasi ya 93 mnamo mwaka 2006 na kushuka mpaka nafasi ya 116 mnamo mwaka 2010 kati ya nchi 178). Licha ya hayo yote, bado hakuna ishara ya dhamira ya serikali kutatua rushwa. Hakuna hata kiongozi mmoja wa ngazi za juu ambaye ameshtakiwa au kufungwa kutokana na makosa ya rushwa. Serikali ya Tanzania haijafanya lolote juu ya wahusika wa kitanzania wa sakata la kesi ya BAE kuwafikisha mbele ya sheria.

Swali linaibuka kwanini watanzania wanasisitiza katika kurejeshwa kwa fedha toka BAE Systems moja kwa moja serikalini.

Hakuna uhaba wa rasilimali Tanzania na endapo Tanzania inapenda kuongeza mapato, inaweza kufanya hivyo kirahisi sana kupitia mifumo sahihi ya kufanya kazi ya kukusanya kodi nchini.

Mfano mzuri ni kupitia sekta ya madini. Tafiti (Kukimbia kwa miguu miwili: Kwanini umaskini unaendelea kuwa mkubwa Tanzania na nini kifanyike iliyoandikwa na Lars Oberg na Amerakoon Bandara Mei 2011; /‘Running with two legs: Why poverty remains high In Tanzania and what to do about it’ written by Lars Oberg and Amerakoon Bandara in May 2011, McCulloch Professor of Economics, Dalhousie University, Nova Scotia, Canada, and Economics Advisor, UNDP, Dar es Salaam, respectively) inasema kwamba endapo kodi katika makampuni “corporate tax” ingelipwa katika mapato ya dhahabu ya Barrick mwaka 2010 kwa kiwango cha asilimia 35 cha Marekani, fedha ambazo zingekusanywa zingekuwa katika ukanda jumla ya Tsh 225 bilioni, ingetosha kuwezesha mifuko ya pensheni kwa watanzania wote walio zaidi ya umri wa miaka 65 kwa kiwango cha Tsh 10,000 kwa mwezi.

Wazi wazi kiasi hiki cha fedha kingeweza kutumika katika njia mbalimbali kwa mchango mkubwa wa kupambana na athari za umaskini. Swali linaibuka kwanini haikuwa hivyo? Ukizingatia kiwango cha hali tete cha rushwa nchini Tanzania, itakuwa ujinga kupendekeza DfID kuhakikisha fedha ambazo zitaliwa na BAE zitatumika vizuri na serikali ya Tanzania.

Tanzania inatafuta uwekezaji wa moja kwa moja toka nje lakini bado imeshindwa kutengeneza mazingira bora. Kushindwa huko kunapunguza mchango wa Uingereza na wahisani wengine kuchochea katika uimarikaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Uwasilishwaji huo unaabatanishwa na ripoti iliyotajwa hapo awali ya Brian Cooksey ambayo iligundua “ubora wa miundo mbinu nchini na taratibu za kiuchumi ni miongoni mwa vigezo vikubwa muhimu katika uwekezaji na mazingira ya kibiashara yanayowakabili wawekezaji wa ndani na wa nje, kwa uchumi kwa ujumla ambao kwa kiasi kikubwa ni wa vijijini na isiyo rasmi”.

Katika kuunga mkono uwasilishaji wa hoja yangu, nina rejea hususan (bila kuacha) kamati katika kesi yetu nchini Tanzania ambayo inafahamika kama kesi ya shamba la Silverdale. Ni kesi ambayo inaweza kusababisha mvuto wa ndani kwa wajumbe wa kamati na serikali ya Uingereza. Inadhihirisha kasoro ya namna ambavyo wawekezaji wa nje wanazokutana nazo nchini Tanzania, kushindwa kwa utawala na mamlaka ya kisheria na kukataa kwa Tanzania kufanyia kazi ujumbe rasmi uliofanywa kwa niaba yetu. Narejea pia kamati kwa mrejeo wa kesi ya shamba la Silverdale, na bwana Edward Clay kwa ushahidi kwa Kamati ya Uchumi ya Bunge la Mabwanyenye ya Uingereza (House of Lords Economic Affairs committee) mnamo Julai 5.

Mnamo 2004, mume wangu Stewart Middleton (mshauri katika masuala ya kilimo na uchumi mwenye zaidi ya uzoefu wa miaka 40 katika umiliki wa shamba dogo ndani ya Afrika) name niliwekeza nchini Tanzania. Kati yetu, tuna zaidi ya miaka 70 ya kuishi, kufanya kazi na kulima nchini Afrika. Tulikodi kwa takribani jumla ya miaka 45 shamba la Silverdale & Mbono lililopo katika wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Mume wangu alipanga kimkakati kulikarabati shamba ili kuweza kupata faida na muendelezo chini ya mpango kabambe wa kilimo cha kibiashara. Kiini cha mpango wake ikiwa ni kukarabati mali ili kuiwezesha kuendelea na kuleta faida katika uendeshaji wake, kujenga uwezo na kuimarisha ujuzi wa watendaji kazi ambayo ingeweza kuendelea kwa muda mrefu wa kipindi chote cha kutumika kwa ardhi. Uzoefu wake wa miaka mingi katika kuendeleza na kusimamia miradi ya mashamba katika jamii tata, zenye mazingira magumu ya kisheria na taratibu katika chumi za nchi zilizoendelea Afrika na mahala pengine kulifanya wazo la Stewart kuwa mtu mahsusi katika kuamsha na kuendeleza mali ile.

Ndani ya miezi sita ya kwanza, ujuzi wa Steward katika kilimo hasa uwekezaji wa kifedha, kutengeneza na kusimamia wafanyakazi ulilibadili shamba toka kuwa shamba lililotekelezwa na lisilozalisha wala kutoa faida kibiashara mpaka kuwa shamba lenye kuzalisha na kumudu kuajiri zaidi ya wafanyakazi wakitanzania 150 toka katika jamii; kuzalisha na kusafirisha nje ya nchi zaidi ya tani nane za maharagwe ya kijani kipindi cha mavuno; na shamba la kwanza nchini Tanzania kuweza kupata utambuzi jumuiya ya ulaya “EUROPGAP accreditation”, uwekwaji wa shamba katika kundi lenye thamani jambo ambalo lingeweza kuturuhusu kupata masoko yenye thamani na faida katika jumuiya ya Ulaya.

Tulikodi shamba toka kwa Benjamin Mengi, kaka wa Reginald Mengi, mtu mwenye ushawishi katika vyombo vya habari kitaifa na kiafrika katika jamii ya kibiashara. Kukodi huko kulizingatia kwa ukamilifu sheria za Tanzania na hakuna mahakama ilitengua kukodi huko.

Bwana Reginald Mengi anashiriki katika bodi mbalimbali za kimataifa na amekuwa mwenyekiti wa bodi ya Tanzania ya biashara, uhasibu na wakaguzi (Chairman of Tanzania’s National Board of Business Accountants and Auditors), mwenyekiti Tanzania wa tawi la kimataifa la chama cha wafanyabiashara (Chairman of Tanzania’s Chapter of the International Chamber of Commerce), na mwenyekiti wa tawi la Tanzania la Jumuiya ya Madola la umoja wa wachapaji (Chairman of the Tanzanian Chapter of the Commonwealth Press Union). Pia ni mjumbe katika bodi ya menejimenti ya baraza la wafanyabiashara wa Jumuiya ya Madola (member of the Board of Management of the Commonwealth Business Council) na pia alishiriki katika kamati ya Blair juu ya Afrika.

Mwaka mmoja baada ya mkataba wetu wa kukodi, Benjamin Mengi alitaka shamba lake lirejeshwe, akidai hakulipwa malipo yake yote. Kwa taarifa, alisaini (Benjamin Mengi) risiti ya kupokea malipo. Tulipokataa kurejesha shamba, alituambia angetutoa ndani ya Tanzania kwa njia yoyote, “kutukata vipande vipande na kutuweka katika jeneza, kama ikilazimu”- kauli aliyoitoa mbele ya mkuu wa polisi wa mkoa katika eneo husika.

Kampeni ya zaidi ya miaka minne ya vurugu na unyanyasaji ilianza dhidi yetu, ambayo iliwezeshwa na polisi na mahakama na pia ikihusisha taasisi za kiserikali kadhaa. Hii ilijumuisha:

  • Kukataa kwa mamlaka husika kusajili hati yetu au kuitambua
  • Kuharibiwa kwa mikataba ya kibiashara
  • Vurugu kwa, na kufungwa wafanyakazi wetu muhimu na
  • Kukamatwa kulikokuwa kunajirudia na kufungwa kwa mume wangu na kupazwa kwa mashtaka.

Kinachoathiri zaidi katika kampeni hii iliyokuwa ikibadilika ilikuwa ni kwa Bwana Mengi kutumia mahakama kutuingiza sisi katika miaka yenye kugharimu na madai yenye uchokozi na kuudhi katika mfumo wenye rushwa wa kisheria ambao ulituathiri kiuchumi na hisia.

Mawaziri wa serikali iliyopita wa Uingereza, Mstahiki Malloch Brown na Margaret Becket pamoja na viongozi wafanyabiashara wa hadhi ya juu na mke wa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, bibi Cherie Blair wote wamewahi kuiwasilisha hii kesi kwa Rais Kikwete. Kwa nyakati tofauti, Rais Kikwete amekuwa akihakikishia sheria na haki itachukua nafasi yake katika kesi hiyo.

Baada ya miaka mitano ya juhudi za ofisi za nje na jumuiya ya madola na makamishna wa ubalozi wa Uingereza Tanzania (British High Commission), Juni 2009 serikali ya Tanzania ilisema tulighushi nyaraka za kukodishwa shamba, hatukulipa kiasi tulichotakiwa kulipa, hatukuwa wawekezaji wa maslahi kwa Tanzania na tulikimbia nchi kutokana na hukumu ya mahakama dhidi yetu. Mtu ambaye alitoa kauli hiyo alikuwa ni balozi wa zamani wa Tanzania nchini Uingereza, kwa sasa balozi nchini Marekani, bibi Mwanaidi Majaar.

Kiini cha kesi yetu kina anika wazi rushwa na kutokuheshimiwa kwa sheria. Chaguo dogo linaikabili serikali ya Tanzania: kusaidia utawala wa kisheria na kulinda maslahi halali ya wawekezaji, au kuwezesha vitendo vya jinai kama ilivyokuwa katika kesi yetu.

Ijapokuwa kwa kiwango cha chini, tulimudu kutoa fursa endelevu za kimaendeleo Tanzania na kuboresha maisha ya watu duni. Tuliikimbia nchi mnamo mwaka 2008 kutokana na kukithiri kwa vitisho dhidi ya uhai wetu na uwepo wa vikundi vya watu wenye silaha katika shamba letu na hivyo kupoteza uwekezaji wote tuliokuwa tumeufanya. Benjamin Mengi, alilivamia shamba, akavunja na kuingia katika nyumba yetu na kuwakamata wafanyakazi wetu waliokuwa wamebaki na kuiba mali zetu zilizokuwa zimebaki. Shamba ambalo tulikuwa tumelikodi kwa sasa lipo wazi tayari kutolewa kwa wawekezaji wengine na tumetendewa kama vile hatukuwahi kuwepo Tanzania.

Namna tulivyofanyiwa si jambo lililopo hewani. Unyanyasaji na vitisho, ukichanganya na matumizi ya nguvu vimekuwa vitu vya kawaida nchini Tanzania. Mamlaka zimeshindwa kulinda haki halali kwa mali na usalama wa watu na inachochea siasa za chuki na kukua kwa kutozingatia sheria.

Hivi karibuni Julai 15, 2011 hali imegeuka kwa jumuiya ya asili ya kiasia Mwanza, Kaskazini mwa Tanzania. Waasia hao ambao walishambuliwa walikuwa wakiongea Kiswahili kizuri na walizaliwa na kukulia Tanzania, ambapo baadhi ya familia za kiasia zimekuwapo nchini kwa zaidi ya miaka 150. Majengo yalishambuliwa, magari mawili kuchomwa moto na mengine kupigwa mawe, likiwemo gari la kuzima moto. Vijana wenye hasira walizunguka mitaani huku wakishambulia kwa mawe nyumba kadhaa zinazokaliwa na watanzania wenye asili ya kiasia. Madirisha ya msikiti wa wahindu hayakusalimika kwa vijana wale, waliharibu kitu chochote ambacho kilikuwa kina milikiwa na waasia. Licha ya kutumika kwa askari wa kutuliza ghasia, kushambuliwa kwa wafanyabiashara wenye asili ya kiasia kuliendelea na wengi walishambuliwa moja kwa moja kimwili na wakati huo maduka yao yakiporwa. (2)

Tabia kama hizo zimeanza kuzoeleka nchini Tanzania. Inavunja haki za kibinadamu za watu nchini-haki ambazo wote wanapaswa kuneemeka nayo, iwe mwananchi au mkazi-na hicho ni kitu ambacho kinairudisha nyuma nchi ambayo inaathiriwa na umaskini uliokithiri, licha ya viwango vya juu vya misaada inayotolewa nchini na kukua kwa uchumi. Kumbukumbu za vitendo kama vya Idd Amin wa Uganda; je tunaweza kupuuza uvunjwaji wa haki za kibinadamu kama kiasi kile?

Kwa heshima nina pendekeza HMG ichochee lengo lake la mipango ya misaada inayoitoa kwa kushinikiza watanzania kutoa wigo mpana wa kulindwa kwa sheria kwa wawekezaji wa ndani na wa nje na kutengeneza mazingira bora ya kutoa imani kibiashara. Kwa sasa, kwasababu mashaka ya kujitosheleza yapo katika hasara inayohusika na kuisaidia serikali ya Tanzania na uwezo wa DfID kuhakiki itakuwa salama na zaidi yenye ufanisi kurudisha fedha za BAE kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali kuliko moja kwa moja serikalini.

Watanzania wa hali duni wanastahili vilichobora zaidi toka katika serikali yao na wahisani. Matumizi mabaya na kushindwa kwa serikali yao kuna waathiri zaidi kuliko chochote. Ninaiasa kamati kukumbuka maneno ya Thomas Rainsborough mnamo mwaka 1647: “Maskini kuliko wote aliyeko Uingereza ana maisha ya kuishi kama yule mwenye uwezo” (Thomas Rainsborough’s words in 1647: “The poorest he that is in England hath a life to live as the greatest he”). Kesi ya shamba letu la Silverdale si maalumu au ya kipekee: maendeleo yatayabadilisha maisha ya watu maskini mpaka hapo rushwa itakapo chukuliwa kwa umakini Tanzania kwa wote serikali ya Tanzania na wahisani. “Kwa bahati mbaya kadiri unavyochimba zaidi katika kesi, ni zaidi unavyogundua. Swali ni je tuna motisha wa kuchimba?” (3)

(1) Public goods, rents and business in Tanzania.
(2) http://www.youtube.com/watch?v=U67rfGzeDV4&sns=em
(3) Sir Edward Clay: The Select Committee on Economic Affairs 5th July 2011.

Na Sarah Hermitage

Muhimu: Makala hii awali ilichapwa kwa lugha ya kiingereza katika mtandao wa www.africanexecutive.com .CTS imeitafsiri kwa lugha ya Kiswahili.

No comments: